Kongamano hilo litasimamiwa na Benki ya Ustawi ya Kiislamu (IDB), Taasisi ya Elimu na Utafiti wa Kiislamu (IRTI), Benki ya Taifa ya Pakistan na Kamisheni ya Elimu ya Juu ya nchi hiyo.
Kongamano hilo litachunguza hali ya sasa ya uchumi na biashara ya Kiislamu na taathira zake katika uchumi wa dunia na kutayarisha fursa za ustawi wa uchumi.
Maudhui nyingine zitakazojadiliwa katika kongamano hilo la kimataifa ni pamoja na njia za uchumi wa Kiislamu za kutatua mgogoro wa sasa wa kimataifa, mafanikio na changamoto zinazukabili uchumi wa Kiislamu, misingi na mbinu za uzalishaji katika mfumo wa uchumi wa Kiislamu, taathira za wakfu katika ustawi wa kijamii na kiuchumi na kupunguza umaskini, masuala ya kisheria yanayohusiana na karadhi na masuala ya riba.
Kandokando ya mkutano huo kutafanyika warsha ya mafunzo kuhusu mbinu za Kiislamu za biashara na bima ya Kiislamu. 735237