Maonyesho hayo yamefunguliwa na mkuu wa Kitivo cha Sanaa katika chuo hicho na kuhuduriwa na wanafunzi wanaosoma kozi za masuala ya Iran.
Maonyesho hayo yamewasilisha Qur'ani zilizotarjumiwa kwa lugha kadhaa duniani, kaligrafia za Qur'ani Tukufu, sanaa zenye maandishi ya Qur'ani kama vile mazulia na kazi za mikono. Aidha maonyesho hayo pia yana michoro ya Ustadh Faraschian na Ustadh Shakiba wa Iran.
Akizungumza katika maonyesho hayo, mkuu wa Kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Addis Ababa amesema Iran na Ethiopia ni nchi zenye staarabu za kale. Amesema tamaduni za kale za Uajemi na Axum zimekuwa na uhusiano wa kirafiki tangu jadi. "Kwa kutegemea uwezo wa vijana wake, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepiga hatua kubwa za kimaendeleo na kuweza kukidhi mahitaji yake ya ndani na hivyo kuifanya nchi hiyo iweze kujitegemea" amesema mkuu wa Kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Addis Ababa.
Maonyesho hayo ya siku tano yaliandaliwa na Idara ya Utamaduni ya Iran nchini Ethiopia na kumalizika Januari 29.
739357