IQNA

ISESCO yaunga mkono mpango wa elimu wa 'Nourul Maarif'

18:13 - February 01, 2011
Habari ID: 2074251
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO limetangaza kuwa litatoa msaada wa kifedha kusaidia Kamisheni ya Taifa ya Elimu na Utamaduni ya Iraq katika mpango wake wa kustawisha elimu uliopewa jina la Nuorul Maarif makhsusi kwa watoto wa kike.
Tovuti ya ISESCO imeripoti kuwa mpango wa Nourul Maarifa ni maksusi kwa ajili ya watoto wa kike wenye umri wa kati ya miaka 8 hadi 12 ambao wamelazimika kuacha shule au hawakufanikwa kwenda shule kabisa kwa sababu moja au nyinine.
Kwa mujibu wa mpango huo ambao unatekelezwa na idara ya masuala ya elimu ya serikali ya Iraq katika shule kadhaa za nchi hio, watoto hao wa kike watapata elimu na mafunzo ya ufundi. 740309


captcha