IQNA

Algeria kuwa mwenyeji wa sherehe za mji mkuu wa kiutamaduni wa Kiislamu

1:26 - February 07, 2011
Habari ID: 2076444
Wizara ya Utamaduni ya Algeria imetangaza kuwa ufunguzi rasmi wa sherehe za kuchaguliwa mji wa Tlemcen kuwa mji mkuu wa kiutamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu zitafanyika tarehe 17 Aprili zikihudhuriwa na wawakilishi wa zaidi ya nchi 40.
Waziri wa Utamaduni wa Algeria amesema kuwa sherehe za kuchaguliwa Tlemcen kuwa mji mkuu wa kiutamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu zitafanyika kitaifa tarehe 12 Rabiul Awwal sambamba na Maulidi ya Mtume Muhammad (saw).
Waziri huyo amekumbusha kwamba sherehe hizo ni fursa ya kubuni kazi za sanaa za aina mbalimbali hususan kwa wasanii wa Algeria.
Amesema sherehe hiyo pia itakuwa na matamasha ya filamu za matukio ya kweli, makundi ya kutumbuiza ya muziki wa asili, maonyesho ya bidhaa mbalimbali na vikao vya mijadala ya historia ya mji wa Tlemcen.
Sherehe za kuteuliwa mji huo kuwa mji mkuu wa kiutamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu zitasimamiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la OIC. 742865

captcha