Tovuti ya Islam Today imeripoti kuwa insiklopedia hiyo ina juzuu sita na kila juzuu ina kurasa 800.
Juzuu ya kwanza hadi ya tatu ya insiklopedia hiyo inazungumzia jinsi Uislamu ulivyostawi na kuenea katika Mashariki ya Kati baada ya kuporomoka ufalme wa Roma Mashariki.
Juzuu ya nne inachunguza utajiri wa jamii na utamaduni wa Kiislamu tangu kudhihiri dini hiyo hadi karne ya 18 na ina makala kuhusu elimu ya irfan, sheria za Kiislamu, fasihi ya Kifarsi, Urdu na Kiarabu, elimu, muziki na mapishi katika ulimwengu wa Kiislamu.
Juzuu ya tano ya insiklopedia hiyo inazungumzia taathira ya udhibiti wa Magharibi katika ulimwengu wa Kiislamu kuanzia karne ya 18 hadi hii leo. Juzuu ya sita inajadili mambo mbalimbali kama uhajiri, mawasiliano, Waislamu barani Ulaya, vyombo vya habari na machapisho na sanaa ya kisasa katika Mashariki ya Kati.
Nakala ya awali ya insiklopedia hiyo ya Chuo Kikuu cha Cambridge ilichapishwa mwaka 1977 katika juzuu mbili.
Insiklopedia mpya ya historia ya Uislamu ya Cambridge imekusanywa na kundikwa katika kipindi cha miongo minne. 743352