Kituo cha upashaji habari cha The News kimeripoti kuwa sherehe za siku tano za Maulidi ya Mtume zitafanyika katika Msikiti wa Faisal wa chuo hicho kwa shabaha ya kueneza amani na utulivu kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume Mtukufu (saw).
Mkurugenzi wa Akademia ya al Daawa Sajid al Rahman amesema kuwa sherehe hizo zitachunguza sehemu mbalimbali za maisha ya Mtume Muhammad (saw) na mafundisho ya Kiislamu ya kuongoza kizazi cha vijana.
Vilevile kutakuwepo maonyesho ya vitabu yatakayoshirikisha makampuni na taasisi za uchapishaji za Pakistan. Sehemu nyingine ya ratiba za sherehe hizo ni kiraa ya Qur’ani Tukufu itakayofanyika katika ukumbi wa IQbal Lahori na kuwashirikisha makarii mashuhuri wa Pakistan. 744495