IQNA

Kongamano la Sira ya Mtume katika Maandiko ya Uholanzi

12:52 - February 12, 2011
Habari ID: 2078751
Chuo Kikuu cha Muhammad bin Abdullah cha Morocco kimepanga kuitisha kongamano la kimataifa la kuchunguza maisha na sira ya Mtume Muhammad (saw) katika maandiko ya Uholanzi. Kongamano hilo limepangwa kufanyika kwa kipindi cha siku tatu katika mji wa Fas yapata miezi miwili ijayo.
Kongamano hilo ni sehemu ya silsila ya vikao vinavyochunguza sira ya Mtume Muhammad (saw) katika vitabu vya Kifaransa, Kiingereza na fasihi ya Kiarabu, maandiko ya Kijerumani na Kihispania na maandiko ya wasomi wa Kimarekani. Vikao hivyo vilianza mwaka 2004 katika Chuo Kikuu cha Muhammad bin Abdullah.
Kongamano hilo litafanyika kuwaenzi waandishi wa Kiholanzi na juhudi zao za kuchunguza maisha ya Nabii Muhammad (saw) na uchunguzi kuhusu masuala ya Mashariki.
Malengo mengine ya kongamano hilo ni kuhamasisha watafiti wa Uholanzi kutalii na kuchunguza sira na maisha ya Mtume Muhammad (saw). 744588




captcha