IQNA

Faharasa ya nushka za maandishi ya Kiislamu kuonyeshwa katika jumba la makumbusho la Foumban

13:20 - February 12, 2011
Habari ID: 2079420
Jumba la makumbusho la Bamoun Royal Palace katika mji wa Foumban nchini Cameroon limepanga kuonyesha faharasa ya nakala za maandishi ya Kiislamu na Kiarabu zinazohifadhiwa katika jumba hilo.
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la OIC (ISESCO) limeripoti kuwa maafisa wa jumba hilo la makumbusho wakishirikiana na shirika la ISESCO mbali na kuonyesha faharasa ya nakala za maandishi ya Kiislamu zinazohifadhiwa katika jumba hilo watatengeneza pia filamu kuhusu nushka hizo.
Mkuu wa Maktaba ya Taasisi ya Kiislamu ya Dakar, Senegal Demba Tiwi ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya hati na maandishi ya mkono na Papa Tumani Ndiya, mtaalamu wa masuala ya utamaduni wa shirika la ISESCO wanashirikiana na wasimamizi wa Bamoun Royal Palace kwa ajili ya kutimiza malengo hayo. 745976
captcha