Uandaaji wa sherehe za ufunguzi wa msikiti huo unashughulikiwa na Jumuiya ya Kiutamaduni ya Mtume Mtukufu (saw) ya mji wa Saihat.
Jumuiya hiyo imewataka wanafikra, wanazuoni na wasomi wa Kiislamu kushiriki kwa wingi katika sherehe ya ufunguzi wa msikiti huo na kutoa mchango na fikra zao kuhusu jinsi ya kufanikisha shughuli zake.
Imesema lengo la kutengwa siku ya Miladu Nabii kuwa siku ya kufunguliwa msikiti huo ni kuambatanisha shughuli zake na sira pamoja na miongozo ya Mtume Mtukufu Muhammad (saw). 747771