IQNA

Kongamano la kidini na kiutamaduni la 'Machipuo ya Ujumbe' kufanyika Karbala

16:54 - February 15, 2011
Habari ID: 2081424
Kongamano la kila mwaka la kidini na kiutamaduni la 'Machipuo ya Ujumbe' litafanyika tarehe 21 hadi 23 huko katika mji mtakatifu wa Karbala, Iraq kwa mnasaba wa kuadhimishwa Maulidi ya Mtume Mtukufu (saw).
Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na idara inayosimamia haram mbili za Imam Hussein na Hadhrat Abul Fadhl Abbas (as) litafanyika chini ya anwani ya 'Mtume Mtukufu wa Uislamu, Mwanadamu Mkamilifu na Mleta Ujumbe wa Urafiki.'
Ali Swaffar mmoja wa wanachama wa kamati inayoandaa tamasha hilo amesema kuwa tamasha hilo litafanyika kwa mnasaba wa kuadhimishwa siku ya kuzaliwa Mtume Mtukufu pamoja na Imam Ja'far al-Swadiq (as) mmoja wa wajukuu wa Mtume (saw).
Amesema shakhisa mbalimbali wa kidini, kiutamaduni na kijamii wa Iraq watashiriki na kutoa hotuba katika tamasha hilo ambalo litajumuisha ratiba mbalimbali za mashairi, burudani na masuala ya sanaa. 748098
captcha