IQNA

Jimbo la Colorado kupata kituo kipya cha utamaduni wa Kiislamu

15:58 - February 16, 2011
Habari ID: 2081938
Kituo cha Kiislamu cha mji wa Boulder katika jimbo la Colorado nchini Marekani kimeanza kuchangisha fedha za kujenga kituo kipya cha utamaduni cha Kiislamu.
Kwa mujibu wa tovuti ya DailyCamera Zaidi ya familia 300 za Kiislamu zinaishi katika mji wa Boulder na msikiti wa sasa katika mji huo ambao una uwezo wa kubeba watu 90 pekee ulijengwa mwishoni mwa mwaka 1970.
Taj Shahid, msemaji wa Baraza la Waislamu wa Boulder anasema kuwa jamii ya Waislamu katika mji huo imeongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni na kwamba hatua za lazima zinapasa kuchukuliwa ili kuwaandalia sehemu ya kufanyia ibada na masuala mengine ya kidini. 748520
captcha