Kwa mujibu wa gazeti la Khaleej Times, msikiti huo ambao utakuwa na uwezo wa kubeba watu 900 utajengwa kwa msingi wa usanifu majengo wa Kiislamu.
Hassan Abdu Rahman Swa'b, mkuu wa Mfuko wa Uwekezaji na Wakfu wa Sharjah amesema kuwa ujenzi wa msikiti huo utakamilika katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu ujao.
Ujenzi wake unakadiriwa kugharimu dirhamu milioni 6 za Imarati. 748816