Kwa mujibu wa tovuti ya waltainfo, sherehe za kuadhimishwa siku hiyo zilifanyika katika msikiti wa Anwar ambapo Haj Said Ghazwa Mkuu wa Baraza Kuu la Masuala ya Waislamu la Addis Ababa, mji mkuu wa nchi hiyo alitoa hotuba.
Huku akisisitiza juu ya juhudi za Waislamu za kufikia maendeleo na ustawi, Haj Ghazwa ametaka kuimarishwa utamaduni wa kuishi pamoja kwa amani Waislamu na wafuasi wa dini nyinginezo. Ethiopia ambayo zamani ilikuwa ikijulikana kwa jina la Habasha ina Waislamu ambao wanaunda thuluthi moja ya wananchi wote wa nchi hiyo. 748831