IQNA

Tamasha la Sera za Mtume, maalumu kwa wanawake wa Kishia wa Saudi Arabia

16:05 - February 16, 2011
Habari ID: 2082122
Kundi la kiutamaduni la al-Fatimiyaat la mjini al-Awamiya katika mkoa wenye wakazi wengi wa Kishia wa Qatif limeandaa tamasha la Sera za Mtume (saw) maalumu kwa wanawake wa Kishia wa Saudi Arabia kwa mnasaba wa kusherehekea Maulidi ya Mtume Mtukufu (saw).
Tamasha hilo lilianza siku ya Jumatatu Februari na litaendelea hadi siku ya Jumapili Februari 20. Makundi mbalimbali ya uimbaji kasida na usomaji mashairi kama ya Lu'lu' al Batul na Dar al-Wadia' yatashiriki kwenye tamasha hilo kwa lengo la kuwatumbuiza washiriki.
Mbali na kutekeleza vipindi mbalimbali vya burudani na furaha, wanawake watakaoshiriki kwenye tamasha hilo pia watatoa hotuba mbalimbali za kumsifu Mtume (saw) na kubainisha fadhila zake za kimaanawi. 748980
captcha