IQNA

Gazeti la Habari za Waislamu lachapishwa Ghana

18:05 - February 16, 2011
Habari ID: 2082219
Gazeti la Habari za Waislamu limeanza kuchapishwa nchini Ghana kwa mnasaba wa maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran.
Tawi la Jumuiya ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu ya Iran likisaidiana na kituo cha utamaduni cha Iran mjini Accra kimezindua gazeti la Habari za Waislamu linalosimamiwa na Umoja wa Wislamu wa Ghana kwa mnasaba wa kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Toleo la kwanza la gazeti hilo limeakisi kazi za kituo cha utamaduni cha Iran katika siku za maadhimisho ya Mapinduzi ya Kiislamu na makala ya Maadili na Akhlaki ya Imam Khomeini. Vilevile limeandika makala mbalimbali kuhusu Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. 749030



captcha