IQNA

18:04 - February 19, 2011
Habari ID: 2083437
Sheikh Ahmad Zein:

Mwamko wa umma wa Kiislamu utashinda kwa kufuata Qur'ani Tukufu

Harakati ya mwamko wa umma wa Kiislamu ndiyo hatua ya kwanza ya kuponya maumivu ya Waislamu na harakati hiyo itafikia ushindi kwa kufuata kikamilifu thamani na misingi ya Uislamu na Qur'ani Tukufu.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuia ya Maulamaa wa Kiislamu wa Lebanon Sheikh Ahmad Zein katika Mkutano wa 24 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu unaofanyika mjini Tehran na kuongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inastahili kupongezwa kutokana na juhudi zake kubwa za kuimarisha umoja na mshikamano wa Kiislamu. Sheikh Zein amesema ulimwengu wa Kiislamu ulikuwa umelala na mwamko wa sasa wa umma wa Kiislamu ni harakati itakayokomesha hali hiyo ya kutuama.
Ameongeza kuwa idadi ya Waislamu hii leo inakadiriwa kuwa bilioni moja na milioni 300 lakini inaumiza mno kuona mwanamke wa Kiislamu akiomba msaada huo Quds Tukufu bila ya kujibiwa na Muislamu yeyote. Amesisitiza kuwa hali hiyo itaondoka kwa umoja na mshikamano wa Kiislamu.
Sheikh Ahmad Zein amesema harakati ya mwamko wa umma wa Kiislamu ndiyo hatua ya kwanza ya kuponya maumivu ya Waislamu na harakati hiyo itafikia ushindi kwa kufuata kikamilifu thamani na misingi ya Uislamu na Qur'ani Tukufu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu wa Lebanon amewataka maulamaa wa Kiislamu kujikomboa kutoka kwenye makucha na vizingiti vinavyowekwa na serikali na kubeba ujumbe halisi wa Uislamu na kuueneza kwa uhuru na pia kutangaza sheria za dini kwa kutegemea Qur'ani Tukufu.
Sheikh Ahmad Zein amesema: "Tumekuwa tukizungumzia vitabu, makala, hadithi na kadhalika ilhali haja kubwa zaidi ya Wislamu ni kutekeleza mambo hayo."
Mwishoni mwa hotuba yake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu wa Lebanon amewataka washiriki katika mkutano wa kimataifa wa umoja wa Kiislamu mjini Tehran kutekeleza kivitendo mafundisho ya dini ya Kiislamu na kushikamana chini ya bendera ya Kiongozi wa Waislamu Ayatullahil Udhmaa Sayyid Ali Khamanei. 750428

captcha