IQNA

Sherehe za Miiladu Nabii kufanyika London

17:51 - February 20, 2011
Habari ID: 2084011
Sherehe za kuadhimishwa kuzaliwa Mtume Mtukufu (saw) zimepangwa kufanyika leo Jumapili katika Kituo cha Kiislamu cha London, Uingereza.
Kwa mujibu wa tovuti ya Ice-el, mgeni wa heshima katika herehe hizo ambazo zimeandaliwa na kutuo hicho cha Kiislamu atakuwa Amina Inloes mmoja wa watafiti mashuhuri wa Chuo cha Kiislamu cha London.
Sherehe hizo zitafanyika katika maktaba kuu ya kituo hicho cha Kiislamu kwa wale wanaozungumza lugha ya Kiingereza.
Kituo hicho vilevile kitaandaa sherehe kama hizo hapo siku ya Jumatatu kwa wale wanaozungumza na kufahamu lugha ya Kifarsi kwa mnasaba wa kuzaliwa Imam Ja'far Swadiq (as). 750851
captcha