IQNA

Kitabu cha "Uislamu na Haki za Binadamu" chachapishwa Qatar

15:13 - February 23, 2011
Habari ID: 2085487
Kamati ya Taifa ya Haki za Binadamu ya Qatar (NHRC) ikishirikiana na Kituo cha Kiislamu na Kiutamaduni cha Qatar (Fanar) vimechapisha kitabu kilichopewa jina la Uislamu na Haki za Binadamu.
Gazeti la Peninsula limeandika kuwa katika kitabu hicho chenye aya nyingi za Qur'ani na hadithi za Mtume Muhammad (saw) kumefanyika jitihada za kurekebisha picha mbaya inayotolewa kuhusu Uislamu na kutayarisha fursa nzuri kwa ajili ya mabadilishano ya kiutamaduni.
Mkurugenzi wa Kituo cha Kiislamu na Kiutamaduni cha Qatar Muhammad Ali al Qamdi amesema uandishi wa kitabu hicho umechukua miezi minne na lengo lake kuu ni kueleza vipengee muhimu vya utamaduni wa Kiislamu na mtazamo wa dini hiyo katika nyanja za haki za binadamu.
Ameongeza kuwa kitabu hicho kimefafanua aya za Qur'ani Tukufu, hadithi za Mtume (saw), Hati ya Umoja wa Mataifa na vipengee vya Ilani ya Haki za Binadamu ya mwaka 1948. 752026
captcha