Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kidini wa Algeria ametangaza habari ya kushiriki wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na wanachuo 40,000 katika mashindano ya mtandao wa intaneti yaliyopewa jina la 'kumetemtea Mtume (saw)'.
Kwa mujibu wa tovuti ya Elmoudjahid Waziri Bou Abdallah Ghulamullah ameashiria mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka na kusema kuwa mashindano ya mwaka huu yalifanyika kwa lengo la kusisitiza nafasi ya wanazuoni katika kuimarisha fikra ya Kiislamu nchini Algeria na hasa katika kuboresha shughuli za Madrasa ya Qur'ani ya Iqra na pia Madrasa ya Tafsiri ya Algeria. Pia amesema mashindano ya mwaka huu yamejumuisha mashindano mbalimbali ya usomaji na hifdhi ya Qur'ani ambapo washindi watashiriki katika mashindano ya kimataifa.
Abdul Aziz Bulkhadim, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Algeria pia amesisitiza umuhimu wa mashindano hayo ya kumtetea Mtume (saw) kutokana na kushirikishwa wanazuoni wa Algeria na kupewa umuhimu nafasi yao ya kielimu na kifiqhi nchini. 752736