Mkutano huo unasimamiwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Marekebisho na Shria ya Misri kwa lengo la kuchunguza mstakbali wa Misri kwa msingi wa sheria za Kiislamu na hali ya mambo ilvyo nchini humo ili wananchi waweze kuendeleza harakati zao kwa maarifa.
Mkutano huo pia unachunguza nafasi ya dini tukufu ya Kiislamu katika mapinduzi ya tarehe 25 Januari nchini Misri.
Wasomi na waanazuoni kadhaa wa Kiislamu watahutubia mkutano huo na kugusia masuala mbalimbali.
Jumuiya ya Marekebisho na Sheria ya Misri ilianzishwa na maulamaa na wasomi wa Kiislamu na inaongozwa na Nasr Farid Wasil. 753319