Maonyesho ya sayansi na ubunifu katika ulimwengu wa Kiislamu yanayojumuisha athari za maandiko ya kielimu na kisayansi ya Waislamu yanafanyika katika jumba la makumbusho la mji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur.
Athari za maandiko ya Waislamu katika kipindi cha kunawiri Uislamu katika nchi za Iraq, Uhispania, Misri, Uturuki, India na maeneo mengine zinaonyeshwa katika maonyesho hayo.
Waziri Mkuu wa Malaysia Najib Tun Razaq amesema kwamba maonyesho ya sayansi na ubunifu katika limwengu wa Kiislamu yanadhihirisha taathira za Uislamu na Waislamu kwa wanadamu.
Maonyesho hayo yanayosimamiwa na maafisa wa jumba la makumbusho la sanaa za Kiislamu la Malaysia yanafanyika kwa lengo la kuarifisha utamaduni wa Kiislamu kama msingi wa ustaarabu wa Magharibi. 754623