IQNA

Maonyesho ya kaligrafia ya Kiislamu na Kiarabu yaanza mjini Jeddah

16:23 - February 28, 2011
Habari ID: 2087807
Maonyesho ya kaligrafia ya Kiislamu na Kiarabu imeanza leo Jumatatu mjini Jeddah Saudi Arabia kwa udhamini wa Taasisi ya Utafiti, Utamaduni, Sanaa na Historia ya Kiislamu IRCICA.
Kwa mujibu wa tovuti ya Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC maonyesho hayo yamefunguliwa na Ekmeleddin Ihsanoglu Katibu Mkuu wa OIC katika makao makuu ya jumuiya hiyo mjini Jeddah.
Taasisi ya IRCICA inayofungamana na OIC inaandaa maonyesho hayo kwa madhumuni ya kuimarisha uelewa wa vitabu vya ustaarabu wa Kiislamu na Kiarabu.
Maonyesho hayo ambayo ni sehemu ya shughuli za vyombo vya habari na utamaduni za Jumuiya ya Nchi za Kiislamu yatafanyika kila siku hadi tarehe 7 Machi. 755061
captcha