IQNA

Warsha ya maana ya zaka kwa watoto wa Ufaransa

17:42 - February 28, 2011
Habari ID: 2088067
Warsha ya elimu ya maana ya zaka kwa watoto wadogo wa Ufaransa imeanza leo katika kituo cha Kiislamu cha Tauhidi katika mji wa Lyon.
Warsha hiyo ya mafunzo itaendelea kwa kipindi cha wiki moja.
Katika warsha hiyo inayosimamiwa na Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu wa Ufaransa pia kutakuwepo vikao vya maswali na majibu kuhusu maudhui ya zaka.
Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu wa Ufaransa ilianzishwa mwaka 1987 katika mji wa Lyon na kundi la vijana wa Kiislamu kwa lengo la kuarifisha Uislamu sahihi na kulinda utambulisho wa kidini wa Waislamu nchini Ufaransa. 755334




captcha