IQNA

Rais wa Ujerumani atembelea jumba la sanaa ya Kiislamu nchini Qatar

16:07 - March 02, 2011
Habari ID: 2089344
Rais Christian Wulff wa Ujerumani akiandamana na mkewe pamoja na ujumbe wake rasmi ametembelea jumba la mambo ya kale ya sanaa ya Kiislamu mjini Doha Qatar.
Kwa mujibu wa gazeti la nchi hiyo la Gulf Times ujumbe huo wa ngazi za juu wa Ujerumani umeweza kufahamu na kujionea kwa karibu sanaa ya mikono ya Waislamu, vitabu adimu vya kale, nuskha za vitabu vilivyoandikwa kwa mkono, kazi za vyuma, vioo, bao na ufumaji wa Kiislamu.
Baadaye rais huyo wa Ujerumani alionana na kuzungumza na Sheikh Hamad bin Jassim bin Jabir ath-Thani, Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar.
Jumba la Mambo ya Kale la Sanaa ya Kiislamu la Qatar lililoko mjini Doha Qatar ni moja ya majumba makubwa zaidi ya mambo ya kale katika ulimwengu wa Kiislamu ambapo athari na mambo ya kale yanayohusiana na hata zama za kabla ya Uislamu na watawala wa ufalme wa Wasasani nchini Iran zimehifadhiwa.
Athari na vitu vya kale vinavyoonyeshwa katika jumba hilo vinathibitisha wazi utajiri mkubwa wa Kiislamu katika karne 13 zilizopita.756094
captcha