Kongamano la "Mtume Muhammad (saw), Kigezo Bora kwa Ajili ya Mashariki na Magharibi" limepangwa kufanyika tarehe 26 Machi chini ya usimamizi wa Kituo cha Semina za Sayansi za Kiislamu cha Cambridge (CISS) nchini Uingereza.
Kongamano hilo litafanyika kwa shabaha ya kuchunguza sira ya Mtume Muhammad (saw) na kuarifisha maisha na shakhsia ya mtukufu huyo ambaye ni kigezo cha kuigwa na wanadamu katika zama na maeneo yote hususan katika dunia ya sasa.
Baadhi ya maudhui zitakazochunguzwa katika kongamano hilo ni Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mtume Muhammad (saw) mwalimu wa wanadamu, Muhammad kiongozi, Muhammad kama mume na baba, Muhammad mwenza na rafiki na Mtume Muhammad mkombozi wa wanadamu. 756533