Kituo cha habari cha Saphirnews kimeripoti kuwa vikao hivyo vitakavyoendelea kwa kipindi cha siku 15 vitafanyika kwa shabaha ya kutoa mafunzo ya utamaduni wa Kiislamu na kubainisha mafundisho ya dini hiyo katika jamii.
Miongoni mwa watakaohutubia vikao hivyo ni Mohammed Ghamgui mhadhiri wa Taasisi ya Kimataifa ya Fikra za Kiislamu ya Paris (IIIT).
Mada nyingine itakayojadiliwa na kuchunguzwa katika vikao hivyo ni maisha ya Nabii Muhammad (saw). 757487