IQNA

Filamu ya "Ardhi Yangu" kuonyeshwa katika Jumuiya ya Utafiti wa Uislamu Paris

21:05 - March 05, 2011
Habari ID: 2090601
Filamu ya "Ardhi Yangu" (My Land) inayozungumzia ardhi ya Palestina ambayo imetengezwa na Nabil Ayouch itaonyeshwa katika jumba la michezo ya kuigiza la Chuo cha Utafiti wa Sayansi za Jamii mjini Paris, Ufaransa.
Filamu hiyo itaonyeshwa kwa ushirikiano wa afisa wa Chuo cha Utafiti wa Sayansi za Kijamii cha Paris.
Filamu ya Ardhi Yangu inajumuisha mahojiano na wazee wa Kipalestina, wakimbizi wa Lebanon na vijana wa Israel wanaoishi katika ardhi za Palestina. Filamu hiyo kwa hakika inasimulia kisa cha historia iliyosahaulika.
Mtayarishaji wa filamu hiyo Nabil Ayouch alizaliwa nchini Ufaransa kutokana na baba Muislamu wa Morocco na mama Myahudi mwenye asili ya Tunisia. 757482


captcha