Kikao kuhusu mbinu mpya za masomo ambacho kimeandaliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO kimepangwa kufanyika tarehe 7 hadi 10 Machi huko Conacry mji mkuu wa Guinea Conacry.
Kikao hicho ambacho kitafanyika kwa ushirikiano wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO, kitachunguza vizuizi vya uboreshaji wa mbinu za masomo na njia za kuimarisha mbinu hizo pamoja na viwango vya masomo.
Washiriki pia watachunguza njia za kuimarisha ushirikiano wa wahadhiri na vyuo vikuu, sekta ya viwanda na pia kutumiwa teknolojia ya kisasa katika mfumo wa masomo kwa madhumuni ya kuimarisha masomo nchini Guinea.
Wahadhiri, wataalamu wa masomo na maafisa wa Wizara ya Elimu ya Guinea pia watashiriki katika kikao hicho.
Zakaria Muhammad Rabbani mwakilishi wa ISESCO pia atahudhuria kikao hicho. 758172