IQNA

Warsha ya mafunzo ya kaligrafia ya Kiislamu kufanyika mjini London

17:51 - March 06, 2011
Habari ID: 2091230
Warsha ya mafunzo ya kaligrafia ya Kiislamu imepangwa kufanyika mjini London tarehe 9 mwezi Aprili katika Chuo cha Utafiti wa Mashariki na Afrika (SOAS) cha Chuo Kikuu cha London.
Kwa mujibu wa tovuti ya Sunni Forum warsha hiyo ya masomo ya muda mfupi itawafahamisha washiriki, sanaa ya kaligrafia ya Kiislamu na pia mbinu za ufundishaji wa sanaa hiyo yenye thamani kubwa ya Kiislamu.
Wakufunzi mashuhuri wa sanaa hiyo kutoka Vyuo Vikuu vya Oxford na Cairo watafundisha na kuzungumza katika warsha hiyo juu ya mbinu na aina tofauti za ya kaligrafia ya Kiislamu. 758842
captcha