Kwa mujibu wa Saphirnews hiyo ilikuwa ni duru ya tatu ya maonyesho ya mitindo na mavazi ya Kiislamu kufanyika katika mji huo kwa ajili ya kuimarisha sekta ya mavazi ya Kiislamu duniani. Maonyesho ya mavazi na mitindo ya Kiislamu maalumu kwa mwaka huu wa 2011 yalihudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi za Uturuki, Jordan, Syria, Malaysia, Thailand na India ambapo mashirika ya utengenezaji na ufumaji nguo zaidi ya 150 yalishiriki na kuwasilisha bidhaa zao katika maonyesho hayo. 758950