Akizungumzia suala hilo Abdul Illah al-Heifi, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Muujiza wa Kielimu wa Qur'ani Tukufu amesema kuwa kongamano hilo linafanyika katika Kituo cha Utafiti wa Kiislamu kinachofungamana na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Uturuki. Amesema viongozi wa ngazi za juu wa serikali ya Uturuki wakiwemo Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kidini na Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kidini wamealikwa kushiriki katika kongamano hilo. Kongamano hilo limeandaliwa kwa madhumuni ya kuchunguza athari za muujiza wa kielimu wa Qur'ani Tukufu na sunna za Mtume (saw) kwa fikra za wanadamu katika nyanja mbalimbali za maisha yao ya kielimu. Abdul Illah al-Helfi amesema kwamba Uturuki imechaguliwa kuwa mwenyeji wa kikao hicho kutokana na nafasi yake ya kistratejia ya kuunganisha ustaarabu wa Kiislamu na wa nchi za Magharibi. 761531