IQNA

Mashindano ya kuchagua msikiti bora zaidi nchini Uholanzi kufanyika

16:28 - March 12, 2011
Habari ID: 2093796
Mashindano ya kuchagua msikiti bora zaidi nchini Uholanzi yatafanyika hivi karibuni kwa lengo la kuarifisha utamaduni na maisha ya Waislamu nchini humo pamoja na kuonyesha kiwango cha uzingatiaji Waislamu misikiti yao.
Kwa mujibu wa tovuti ya Muhit, misikiti kumi tayari imewekwa mbele ya washindani ili kuchagua msikiti bora zaidi kati ya hiyo. Kamati inayojumuisha wasanifu majengo na wataalamu katika uwanja huo itaitembelea misikiti hiyo hivi karibuni ili kuainisha ubora wa usanifu majengo uliotumika katika ujenzi wa misikiti hiyo. Nafasi ya maimamu na wahubiri wa misikiti hiyo katika kutoa mafundisho bora zaidi ya Kiislamu na hamu yao ya kuwashawishi Waislamu wajishughulishe na masuala mbalimbali katika jamii ya Uholanzi ni baadhi ya mambo yatakayozingatiwa katika kuchaguliwa msikiti bora zaidi nchini humo. 761552
captcha