IQNA

Kongamano la Mawaziri wa Utamaduni wa nchi za OIC kufanyika Algeria

13:57 - March 13, 2011
Habari ID: 2094541
Mkutano wa kutayarisha kikao cha mawaziri wa utamaduni wa nchi za Kiislamu utafanyika katika mji mkuu wa Algeria Algiers mnamo 16-17 Machi kwa ushirikiano wa Shirika la Kiislamu la Elimu Sayansi na Utamaduni ISESCO, Makao Makuu ya Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC na Wizara ya Utamaduni ya Algeria.
Mkutano huo utajadili matayarisho yanayotakikana kufanikisha kongamano la Saba wa Mawaziri wa Utamaduni wa Nchi za Kiislamu utakaofanyika Novemba 28-29 mwaka huu mjini Tlemcen nchini Algeria. Kongamano hilo linafanyika kwa mnasaba wa mji wa Tlemcen kuteuliwa kuwa Mji Mkuu wa Utamaduni wa Kiislamu katika nchi za Kiarabu mwaka 2011.
ISESCO itawakilishwa katika mkutano na mkuu wake wa utamaduni na mawasiliano Bw. Najib Rhiati.
761838
captcha