IQNA

15:21 - March 13, 2011
Habari ID: 2095000

Umati mkubwa wa Mashia waandamana mashariki mwa Saudi Arabia

Miji tofauti yenye wakazi wengi wa Kishia nchini Saudi Arabia siku ya Jumamosi ilishuhudia maandamano makubwa ya Mashia licha ya kuchukuliwa hatua kali za usalama na askari wa utawala huo wa kifalme kwa ajili ya kuyazuia.

Waandamanaji 19 walitiwa nguvuni na askari hao. Waandamanaji katika maandamano hayo yaliyoanzia katika Msikiti wa Umat al-Baqee katika mji wa al-Hufuf walipiga nara za kutaka kuachiliwa huru wafungwa wanaozuiwa katika jela za Saudia tokea miaka 16 iliyopita bila kufikishwa mbele ya mahakama kwa tuhuma za kuhusika ni mlipuko wa bomu katika kituo cha kijeshi cha Marekani huko katika mji wa Khubar.
Askari usalama wa Saudi Arabia walitumia nguvu za ziada kwa lengo la kuvunja maandamano hayo ambapo mtu mmoja alijeruhiwa na wengine 19 akiwemo Sheikh Ali al-Waili kutiwa nguvuni.
Miji ya Mashia ya Qatif, Safawi, Awamia na Ummul Humaam ilishuhudia maandamano ya maelfu ya watu waliotaka kuachiliwa huru kwa wafungwa wote wa kisiasa. 761871
captcha