IQNA

15:14 - March 14, 2011
Habari ID: 2095757

OIC yafungua ofisi ya uratibu wa masuala ya kibinadamu

Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC imeamua kufungua ofisi ya uratibu wa misaada ya kibinadamu ya Kiislamu katika mji wa Benghazi ulioko mashariki mwa Libya ambao unakabiliwa na maafa makubwa ya kibinadamu

Taarifa ya OIC imesema kuwa ufunguzi wa ofisi hiyo umefanyika kwa mashauriano na Kamati ya Kiislamu ya Jumuiya ya Kimataifa ya Hilali Nyekundu.
Taarifa hiyo imesema kuwa lengo la kufunguliwa ofisi hiyo ni kuendesha shughuli za misaada ya kibinadamu, kukusanya habari na ripoti kuhusu hali ya masuala ya kibinadamu nchini Libya na kutathmini kiwango cha mahitaji ya watu wa eneo hilo.
Jumuiya ya Nchi za Kiislamu imetangaza kuwa ofisi makhsusi ya uratibu wa shughuli za misaada ya kibinadamu ya Kiislamu itafanya kazi ya kutuma misaada, na kuigawa katika maeneo yaliyoathiriwa na mapigano ya ndani nchini Libya kwa kusaidiana na nchi wanachama wa OIC, jumuiya za misaada ya kibinadamu na taasisi za kimataifa.
Vlevile mwakilishi wa Umoja wa Mataifa ameelekea Libya kutathmini mahitaji ya misaada ya kibinadamu na kukagua uwezekano wa kupelekwa misaada kwa walioathiriwa. 763514
captcha