IQNA

15:31 - March 14, 2011
Habari ID: 2095764

Maulama wa Kishia wa Saudia wataka kufanyika marekebisho ya kisiasa

Mulama wa Kishia wa maeneo yenye wakazi wengi wa madhehebu ya Shia huko mashariki mwa Saudi Arabia wamelaani ufyatuaji risasi wa askari usalama dhidi ya waandamanaji wa Kishia na wametoa wito wa kufanyika marekebisho ya kisiasa nchini humo.

Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya mji wa al Rabiiyya katika mkoa wa Qatif Sheikh Abdul Karim al Habiil amelaani kitendo hicho cha polisi cha kuwalenga waandamanaji kwa risasi na ametoa wito wa kuachiwa huru wafungwa wa Kisiasa wanaoshikiliwa katika korokoro za nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 16 kwa tuhuma za kulipua kambi ya jeshi la Marekani.
Amesema serikali ya Riyadh inapaswa kutekeleza matakwa ya wananchi na kuacha kutumia silaha katika kukabiliana na wananchi wanaoandamana.
Sheikh Hashim al Salman wa Saudi Arabia pia ameashiria umuhimu nafasi ya vijana katika maandamano ya amani ya kutaka marekebisho na kusema Waislamu wa madhehebu ya Shia wanasumbuliwa na ukosefu wa uhuru wa kidini na kiraia ambao unapaswa kutekelezwa kwa usawa kati ya raia wote wa nchi hiyo. 763407

captcha