IQNA

Isesco kuandaa kikao cha walimu wa lugha ya Kiarabu huko Istanbul

13:18 - March 16, 2011
Habari ID: 2096492
Kikao cha walimu wa lugha ya Kiarabu kimepangwa kufanyika mjini Istanbul Uturuki kikisimamiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC.
Kikao hicho kimepangwa kufanyika tarehe 17 hadi 20 Machi. Warsha mbalimbali za masomo kwa kutumia mbinu tofauti za kisasa zitafanyika pambizoni mwa kikao hicho cha siku nne.
Mbinu tofauti za kueneza thamani na utamaduni wa Kiislamu kupitia masomo na lugha ya Kiarabu ni baadhi ya masuala yatakayojadiliwa katika kikao hicho. 763911
captcha