IQNA

17:00 - March 16, 2011
Habari ID: 2097110

Kituo cha wataalamu wa uchumi wa Kiislamu chaanzishwa Ubelgiji

Kito cha wataalamu wa uchumi wa Kiislamu (ISFIN) Kimeanzishwa nchini Ubelgiji kama kanali ya kwanza ya kimataifa ya wataalamu wa uchumi wa Kiislamu. Kituo hicho kimeanzishwa na jumuiya 15 za kisheria za Ubelgiji.

Mtandao wa Trends.rnews umeripoti kuwa lengo la kuanzishwa kituo hicho ni kuasisi mtandao wa wataalamu watakaobadilishana uzoefu na tajiriba katika masuala ya uchumi wa Kiislamu na kutumia tajiriba hiyo katika masoko ya kieneo.
Kikao cha kwanza cha kituo hicho kitafanyika mwezi ujao huko Luxembourg na tawi lake jipya litafunguliwa Mashariki ya Kati likishirikisha karibu wanachama 60.
Viongozi wa kituo hicho wanasema moja ya kazi zake ni kuvutia wawekezaji ili wawekeze katika nchi zinazofanyakazi katika medani ya uchumi wa Kiislamu.
Taasisi za Thierry Afschrift ya Ubelgiji, Gide Loyrette Nouel ya Ufaransa, Cuatrecasas ya Uhispania, Arendt & Medernach ya Luxembourg, Morais Leitao ya Ureno na Chiomenti ya Italia ni wanachama katika kituo hicho. 763913
captcha