IQNA

Maonyesho ya Historia ya Makka yamalizika huko Saudia

10:46 - March 29, 2011
Habari ID: 2098770
Maonyesho ya Historia ya Makka ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa wiki moja katika hoteli ya as-Shuhadaa huko katika mji mtakatifu wa Makka yalimalizika siku ya Jumapili.
Maonyesho hayo yalifanyika pambizoni mwa mashindano ya kimataifa ya hifdhi ya Qur'ani kwa wanajeshi, ambayo yalisimamiwa na Idara ya Masuala ya Kidini ya Askari Jeshi ya Saudia. Picha za kale za Masjidul Haram, mji wa Makka, nuskha za kale za Qur'ani na vitu vingine vya sanna ya Kiislamu kuhusu mji huo vilionyeshwa katika maonyesho hayo. 766721
captcha