IQNA

13:31 - April 03, 2011
Habari ID: 2099805

Kazi za Wasomi wa Kiislamu kuhuishwa

Wizara ya Masuala ya Kidini ya Algeria imesema kuna mipango ya kurekebisha maandisi ya wanazuoni wa Kiislamu wa kaskazini mwa Afrika ili kuhuisha turathi ya kidini na kihistoria ya turathi ya Kiislamu katika eneo hili.

Mradi huo utatekelezwa katika fremu ya programu za wizara hiyo za kuadhimisha kuteuliwa mji wa Tlemcen kama Mji Mkuu wa Utamaduni katika Ulimwengu wa Kiislamu mwaka 2011.
Mradi huo utajumuisha maandishi ya wasomi waliokuwa na nafasi muhimu katika kueneza Uislamu barani Afrika kama vile Sheikh Al Maghili, Sheikh Ahmad Hamani, Sheikh Al Wansharisi na Sheikh Abdul Rahman Al Tha’alabi.
Aidha yatachapishwa matoleo ya kale ya jarida la Islah yanayojumuisha makala ya kielimu na fatwa.
Waandalizi wa mradi huo wanaamini kuwa utakuwa na nafasi muhimu katika kuwapa vijana marejeo muhimu ya vitabu vitakavyowawezesha kufahamu historia na utamaduni wa Kiislamu.
767778
captcha