Michoro na maandishi mbalimbali ya aya za Qur'ani Tukufu, sunna za Mtume (saw), dua na mashairi kwa lugha za Kiarabu na Kifarsi yanaonyeshwa katika maonyesho hayo. Kaligrafia hiyo ya Kiislamu imepambwa kwa maandishi na kazi za mikono za kuvutia na hasa zile zinazohusiana na utumiwaji wa maji ya dhahabu katika maandishi ya sanaa hiyo ya Kiislamu. Maonyesho hayo yamepangwa kumalizika tarehe 9 Aprili. 768572