IQNA

Mpango wa 'Ujue Uislamu' watekelezwa katika Chuo Kikuu cha Harvard

17:47 - April 05, 2011
Habari ID: 2101147
Mpango wa 'Ujue Uislamu' umeanza kutekelezwa leo Jumanne katika Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kiislamu ya chuo hicho.
Kwa mujibu wa tovuti ya hcs.harvard, jumuiya hiyo itatekeleza vipindi na ratiba tofauti za kuwaelimisha watu kuhusiana na mafundisho sahihi ya Uislamu na pia kujaribu kuondoa picha mbaya uliyopo katika jamii ya Marekani kuhusiana na Uislamu na Waislamu, kupitia mpango huo utakaoendelea kwa muda wa mwezi mmoja. Baadhi ya mambo yatakayotekelezwa katika mpango huo ni pamoja na kuonyeshwa filamu inayohusiana na hijabu, vikao kuhusu Uislamu, dhifa ya chakula cha jioni ambayo itawawajumuisha wanachuo wa vyuo tofauti vya Marekani na pia usomaji wa mashairi ya Kiislamu. Mwaka uliopita jumuiya ya Kiislamu ya Chuo Kikuu cha Harvard pia iliandaa mpango kama huo ambapo Uislamu uliarifishwa kwa wasioufahamu vyema. 769175
captcha