Akizungumza na wawakilishi wa Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu yaani Bunge la Iran Dakta Mahmoud Ahmadinejad amesema mwanzoni mwa mwaka uliopita, maadui, ambao walishindwa kukabiliana na mantiki yenye nguvu ya taifa la Iran waliamua kutumia maazimio ya Umoja wa Mataifa na vikwazo walivyoviita wenyewe vya kuifanya Iran ipooze kabisa; hata hivyo subira na kusimama imara kwa taifa la Iran kulivigeuza vikwazo hivyo kuwa fursa ya maendeleo kwa taifa hili. Rais Ahmadinejad amefafanua kuwa licha ya njama zilizofanywa na maadui katika mwaka uliopita, ambapo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 50 iliyopita asilimia 20 ya pato la mafuta ya Iran lilizuiliwa, mageuzi makubwa kabisa katika historia ya nchi hii, yaani Mpango wa Utoaji Ruzuku kwa Uadilifu, yaliweza kufanyika kwa upendo na mshikamano wa viongozi na wananchi.../
769613