IQNA

Filamu ya kweli kuhusu mwanakaligrafia bora wa Kiislamu duniani kutengenezwa

12:06 - April 07, 2011
Habari ID: 2101964
Filamu ya kweli kuhusu mwanakaligrafia bora zaidi wa ulimwengu wa Kiislamu duniani itatengenezwa hivi karibuni na Shirika la Chapa na Usambazaji wa Qur'ani Tukufu la Mfalme Fahd mjini Madina.
Kwa mujibu wa gazeti la ar-Riyadh filamu hiyo itabainisha matukio ya sanaa ya kaligrafia ya Qur'ani Tukufu tokea wakati wa Mtume (saw) hadi zama hizi. Filamu hiyo ya dakika thelathini itajaribu kubainisha kwa muhtasari matukio hayo kwa lugha mbili za Kiarabu na Kiingereza. Mbali na lugha mbili hizo filamu hiyo pia itatarjumiwa kwa lugha ya ishara ili iweze kuwanufaisha pia viziwi. Nuskha zote za Qur'ani zitakazoonyeshwa kwenye filamu hiyo ni zile zilizoandikwa kwa mkono. Maondeleo yaliyopatikana katika uwanja wa kaligrafia katika kipindi cha zaidi ya karne moja iliyopita yatabainishwa kwa muhtasari katika filamu hiyo fupi. Kongamano kubwa la wanakaligrafia wa Kiislamu kutoka pembe zote za dunia linatarajiwa kufanyika huko mjini Madina kati ya tarehe 26 Aprili hadi 2 Mei mwaka huu ili kufanikisha juhudi za utengenezaji wa filamu hiyo. 769894
captcha