Kwa mujibu wa tovuti ya Islamic Art Magazine nguo na ufumaji wa kale wa Kiislamu unaohusiana na karne za 14 hadi 19 Milaadia kutoka pembe zote za dunia utaonyeshwa katika maonyesho hayo. Nguo na ufumaji wa falme za Misri, Hipania ya Kiislamu, Wamogholi nchini India, Wasafawi nchini Iran na Waothmani huko Uturuki utaonyeshwa kwa mara ya kwanza katika maonyesho hayo. Maonyeshoa hayo ambayo yameandaliwa kwa ajili ya kuonyesha umuhimu wa nguo na ufumaji katika maisha ya kiuchumi na kijamii ya Waislamu yatamalizika tarehe 6 Mei. 771236