IQNA

Warsha ya utafiti wa Kiislamu yafanyika Uingereza

17:44 - April 13, 2011
Habari ID: 2105485
Warsha ya utafiti wa Kiislamu imepangwa kufanyika tarehe 26 mei huko katika Chuo Kikuu cha Leeds nchini Uingereza.
Warsha hiyo imeandaliwa na kitengo cha utafiti wa Kiislamu cha chuo cha masomo ya juu ch Uingereza. Warsha hiyo itakuwa fursa nzuri kwa wahadhiri wanaofundisha masomo yanayohusiana na Uislamu kujumuika pamoja na kujadili njia za mafunzo hayo katika vituo vya elimu ya juu. Masuala kama vile ya utafiti wa Kiislamu kaskazini mwa Uingereza; hali ya hivi sasa na ya baadaye yatapewa umuhimu katika warsha hiyo. Jumuiya ya Islamic Studies Network pia imeandaa warsha kama hiyo huko Scotland na sehemu nyinginezo za Uingereza. 773755
captcha