Wakati huohuo kikao kingine kama hicho maalumu kwa viongozi wa vituo vya Kiislamu, maimamu wa swala za jamaa na wahubiri wa Kiislamu kiliandaliwa na baraza hilo siku hiyohiyo ya Jumapili katika mji wa Turin Italia.
Vikao vingene vitatu vya kujadili uhusiano wa Waislamu na wasio Waislamu katika kivuli cha mafundisho ya Qur'ani Tukufu na Suna za Mtume (saw), warsha za mbinu bora na Waislamu na ukisasa vimeandaliwa na Jumuiya za Kiislamu za Piemont na Ligurie za Italia. Baraza lililotajwa la maulama wa Kiislamu mwezi uliopita wa Februari pia liliandaa kikao cha siku tatu huko mjini Rome kwa ajili ya kuwafahamisha Waislamu utamaduni na ustaarabu wa nchi za Ulaya ambapo maimamu na wahubiri wa Kiislamu kutoka miji tofauti ya Italia walishiriki. 775801