IQNA

Sira ya Mtume katika maandishi ya Waholanzi kuchunguzwa

17:43 - April 26, 2011
Habari ID: 2112625
Kikao cha kimataifa cha kuchunguza "Sira ya Mtume katika Maandishi ya Wataalamu wa Masuala ya Mashariki wa Kiholanzi kimeanza katika mji wa Fas nchini Morocco.
Kituo cha habari cha jumuiya ya ISESCO kimeripoti kuwa lengo la kikao hicho ni kuchunguza vitabu na maandishi ya wataalamu wa masuala ya Mashariki wa Kiholanzi kuhusu maisha ya mtu binafsi na kijamii pamoja na mwenendo wa Mtume Muhammad (saw).
Mambo mengine yatakayochunguzwa katika kikao hicho ni pamoja na nafasi ya Mtume Muhammad (saw) katika fasihi ya Uholanzi na historia ya kutiliwa maanani maisha ya mtukufu huyo katika fasihi na duru za utafiti za Uholanzi.
Mkutano huo unahudhuriwa pia na Sayyid Muhammad bin Saleh ambaye anawakilisha Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu. 781307
captcha