IQNA

Siku ya Milango ya Wazi ya Uislamu" kufanyika Lyon Ufaransa

18:18 - April 27, 2011
Habari ID: 2113366
"Siku ya Milango ya Wazi ya Uislamu" imepangwa kufanyika tarehe 30 Aprili katika mji wa Lyon nchini Ufaransa.
Kituo cha upashaji habari cha Shatibi kimeripoti kuwa siku ya Milango ya Wazi ya Uislamu itafanyika mjini Lyon kwa lengo la kuwaelimisha wananchi kuhusu shughuli za Kituo cha Kiislamu cha Tauhidi na tawi la taaluma za kidini la al Shatibi.
Katika siku hiyo watu watakaotembelea kituo hicho watakutana na kuzungumza na wanafunzi na wafanyakazi wa sehemu mbalimbali za kituo cha Tauhid na kupewa fursa ya kujiandikisha kwa ajili ya mwaka wa masomo wa 2011.
Vilevile kutakuwepo mashindano ya Ujue Uislamu na uchunguzi wa kiwango cha utambuzi wa elimu ya tajwidi.
Kituo cha al Shatibi hutoa elimu ya lugha ya Kiarabu, kiraa ya Qur'ani na taaluma ya fiqhi ya Kiislamu kwa kipindi cha miaka mitatu kwa kutumia walimu na wataalamu wa masuala ya Kiislamu. 782355
captcha