IQNA

18:38 - April 27, 2011
Habari ID: 2113372

Wanawake wa Iran kuandamana Ijumaa kulaani jinai zinazoendelea Bahrain

Wanawake wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wataandamana baada ya sala ya Ijumaa wiki hii kuwaunga mkono wanawake wenzao wa Bahrain wanaokandamizwa na vikosi vya utawala wa kifalme nchini humo.

Maandamano hayo yameandaliwa na Shirika la Kutangaza Uislamu. Shirika hilo limetoa taarifa likilaani jinai dhidi ya wanawake na mabanati wa Bahrain ambazo zinatekelezwa na vikosi vya utawala wa kifalme nchini humo vikisaidiwa na wanajeshi wa Saudia.
Wakati huo huo Tume ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Bunge la Iran imeitisha kikao kujadili matukio ya Bahrain. Msemaji wa Tume hiyo Kazem Jalali amesema uingiliaji wa kijeshi nchini Bahrain umezidisha mgogoro nchini humo.
Huku hayo yakijiri balozi mdogo wa Bahrain mjini Tehran ameitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran baada ya katibu wa pili katika Ubalozi wa Iran nchini Bahrain kufukuzwa. Afisa huyo wa Bahrain amefahamishwa malalamiko makali ya Iran kuhusu tuhuma zisizo na msingi dhidi ya mwanadiplomasia hiyo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Mkuu wa Idara ya Ghuba ya Uajemi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekosoa vikali hatua ya watawala wa Bahrain kuwakandamiza wananchi wanaotaka demokrasia nchini humo.
782367
captcha